Sunday, January 8, 2012
MILAN WAFIKIA MUAFAKA NA TEVEZ.
KLABU ya AC Milan imefikia makubaliano na Carlos Tevez na sasa wanasubiri kusikia kiasi cha pesa ambacho klabu yake ya Manchester City itataka kwa ajili ya kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Argentina. Akihojiwa na waandishi wa habari jijini Milan Ofisa Mkuu wa timu hiyo Adriano Galliani amesema kuwa wameshafikia makubaliano na Tevez lakini sio City na pia akaongeza kuwa mshambuliaji wake Alexandre Pato hatauzwa kwa ajili ya Tevez. Hatahivyo City tayari wameshakataa toka mwanzo kwa Milan kumchukua mchezaji huyo kwa mkopo wakidai kuwa wnachotaka ni kumuuza mchezaji moja kwa moja. Vyombo vya habari vya Italia jana vilidai kuwa mahasimu wakubwa wa AC Milan klabu ya Inter Milan nao wameingi katika mbio za kumuwania mchezaji huyo kwa kutenga kiasi cha euro milioni 25 kwa ajili ya kumnasa mchezaji huyo mwenye miaka 27.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment