Saturday, January 7, 2012
BALLACK KUACHANA NA LEVERKUSEN MSIMU HUU.
Kiungo wa Bayer Leverkusen Michael Ballack huenda akaachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu lakini bado hajafikiria kustaafu kucheza soka. Akihojiwa hivi karibuni Ballack amesema kuwa alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu ambapo baada ya hapo amedai kuwa nahitaji kufanya kitu tofauti. Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani ameonyesha nia ya kuendelea ya kusakata kabumbu kwa miaka mingine miwili au mitatu kutegemea na kiwango chake kitakavyokuwa. Pamoja na Leverkusen kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu nchini Ujerumani ikiwa katika nafasi ya sita Ballack ameisaidia timu hiyo kwa kiasi kikubwa kuingia katika hatua ya timu 16 bora katika michuano ya Klabu Bingwa ya Ulaya ambapo mwezi ujao watapambana na Barcelona.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment