NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon Rigobert Song amerejea katika kikosi hicho pasipo kutegemewa akiwa kama kocha wa timu hiyo. Song ambaye mashabiki wa soka nchini humo walikuwa wakimwita nahodha mzalendo alitundika daruga baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 iliyofanyika nchini Afrika Kusini. Song ambaye anafananishwa na wachezaji wengine wa timu hiyo kama Bell Joseph Antoine, Eugene Ekeke na Patrick Mboma ambao nao kwa muda mrefu wamekuwa wakiitamani nafasi hiyo.
Uteuzi huo ulifikiwa na kikao cha Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka nchini humo-Fecafoot ambacho mbali na mambo mengine pia kilibadilisha adhabu za wchezaji Samuel Eto’o, Eyong na Assou Ekotto.
No comments:
Post a Comment