Monday, January 9, 2012

FIFA BALLON D'OR 2011 AWARDS: MESSI, GUARDIOLA WAIBUKA KIDEDEA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi ambaye pia anaichezea klabu ya Barcelona ya nhini Hispania amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama BALLON D’OR inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Messi anakuwa mchezaji wa pili kushinda tuzo hiyo mara tatu mfululizo kuanzia mwaka 2009, 2010 na 2011 mwingine akiwa mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Michel Platin aliyewahi kushinda kushinda tuzo hiyo mwaka 1983, 1984 na 1985. 
Katika kinyang’anyiro hicho Messi alikuwa akichuana vikali na mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na mchezaji mwenzie wanaotoka timu moja ya Barcelona Xavi Hernandez. Katika tuzo hizo pia kocha wa Barcelona Pep Guardiola alichaguliwa kuwa kocha bora akiwazidi kina Sir Alex Ferguson wa Manchester United na Jose Mourinho wa Real Madrid waliokuwa wakigombea truzo hiyo. Tuzo zingine zilizotolewa ni pamoja na mchezaji bora wa dunia kwa upande wa wanawake ambay ilikwenda nahodha wa timu ya taifa ya wanawake ya Japan Homare Sawa huku kocha bora a timu za wanawake ilienda pia kwa kocha wa timu hiyo Norio Sasaki na bao bora la mwaka likiwa limefungwa na mshambuliaji wa Santos Neymar.

No comments:

Post a Comment