Friday, March 16, 2012

ABIDAL KUPANDIKIZWA INI JINGINE.

MCHEZAJI wa Barcelona Eric Abidal anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini katika wiki chache zijazo ambapo klabu hiyo imesema upandikizaji huo umekuja toka alipoanza matibabu mwaka mmoja uliopita. Beki huyo wa kimataifa kutoka Ufaransa aliondolewa uvimbe katika ini lake Machi 17 mwaka 2011 na kurejea uwanjani mwishoni mwa msimu huo na kuonyesha athari chache kupotea toka kipindi hicho. Abidal mwenye umri wa miaka 32 alichaguliwa kunyanyua Kombe la Klabu Bingwa Ulaya katika Uwanja wa Wembley msimu uliopita baada ya kuisaidia Barcelona kuisambaratisha Manchester United kwa mabao 3-1 katika mchezo wa fainali. Mchezaji huyo amekuwa mchezaji tegemeo wa Barcelona toka alipojiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Lyon mwaka 2007 ambapo kwasasa nafasi yake ya kucheza michuano ya Ulaya iko mashakani kutokani kutokana na tatizo lake hilo.

No comments:

Post a Comment