Friday, March 30, 2012

BERLUSCONI AKIRUDIA KITI CHAKE MILAN.

WAZIRI Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi amekalia rasmi kiti chake cha urais wa klabu ya AC Milan ya nchini humo baada ya kujiuzulu uongozi wan chi hiyo Novemba mwaka jana. Taarifa kutoka klabuni hapo imetangaza kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo ilimteua Berlusconi kama rais wa heshima wa klabu hiyo. Siku zote Berlusconi amekuwa akikaimu nafasi ya urais wa klabu hiyo, ingawa makamu wa rais Adriano Galliani amekuwa akiiendesha klabu hiyo kwa shughuli za kila siku. Kiongozi huyo wa zamani wa nchi hiyo ambaye alijiuzulu kutokana na matatizo ya kiuchumi yaliyoikumba Italia mwaka jana amewahi kuwa rais wa Milan kutoka mwaka 1986 mpaka 2004 na kurudia tena nafasi hiyo mwaka 2006 mpaka 2008. Katika hatua nyingine mshambuliaji wa klabu hiyo Antonio Cassano ameanza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake kwa mara ya kwanza toka alipofanyiwa upasuaji mdogo wa moyo Novemba mwaka jana ingawa bado anahitaji kupona zaidi ili aweze kucheza na hata kuwa na muda wa kujiunga na kikosi hicho katika michuano ya Klabu Bingwa ya Ulaya.

No comments:

Post a Comment