Friday, March 30, 2012

MADRID KUFUNGUA ACADEMY CHINA.

VIGOGO wa Ulaya, Real Madrid wako mbioni kufungua shule ya soka nchini China mwakani, wakiungana na klabu ya Ligi Kuu ya China, Guangzhou Evergrande, taarifa ambayo imetolewa na mmiliki klabu hiyo ya China katika tovuti yake. Madrid, ambao ni mabingwa mara nyingi zaidi Ulaya, wakiwa wameshinda kombe hilo mara tisa, wako katika mpango wa kujitangaza zaidi na wameingia China, ambayo inavutia klabu nyingine kubwa Ulaya. Shule hiyo itakayokuwa kusini mwa jiji la Guangzhou, itakuwa na wachezaji wapatao 3,000 katika mwaka wa kwanza, watakaokuwa wakitumia vifaa na kufundishwa kwa ubora ule ule wa shule ya Real Madrid nchini Hispania. Kocha wa vijana wa klabu hiyo ya Hispania, Fernando Sanchez Cipitria ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi.

No comments:

Post a Comment