Friday, March 30, 2012

SENEGAL MGUU NJE MGUU NDANO OLIMPIKI.

SIMBA wa Teranga, Senegal watamenyana na Oman katika mechi maalum ya kuwania tiketi ya kucheza Olimpiki mwaka huu, London, mchezo utakaofanyika Aprili 23 mjini Coventry. Mechi hiyo itaamua timu ya mwisho ya kukamilisha idadi ya timu 16 za kucheza Olimpiki inayotarajiwa kuanza Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka huu. Simba wa Teranga wamepata nafasi hiyo baada ya kushika nafasi ya nne katika michuano ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 23 iliyofanyika Morocco Desemba mwaka jana. Oman inayofundishwa na Mfaransa, Paul Le Guen walipata nafasi hiyo baada ya kuifunga Uzbekistan 2-0 Alhamisi katika mechi ya mwisho ya kuwania kufuzu kucheza fainali hizo kwa bara la Asia. Gabon, Morocco Misri ni wawakilishi wengine wa Afrika kwenye Olimpiki ya mwaka huu. Timu nyingine zilizofuzu ni mbali na wenyeji Uingereza, ni kwa upande wa bara ya Asia ni Korea Kusini, Japan, Falme za Kiarabu, huku Brazil na Uruguay ikiwakilisha Amerika Kusini, wakati Uswisi, Hispania na Belarus wakiwakilisha Ulaya na New Zealand wakiwakilisha OCEANIA. Wawakilishi wengine wawili watatoka Amerika Kaskazini, michuano yao inatarajiwa kumalizika Jumatatu ijayo.

No comments:

Post a Comment