Friday, March 30, 2012

MARADONA BLASTS 'COWARDS' AFTER WIFE ATTACK.

KOCHA wa klabu ya Al Wasl ya Muungano wa Falme za Kiarabu-UAE amewashambulia mashabiki wa huko na kuwaita waoga baada ya kulazimika kukimbilia jukwaani kumuokoa rafiki yake wa kike ambaye alikuwa akishambuliwa na mashabiki wenye hasira. Nguli huyo wa soka wa zamani kutoka Argentina alishuhudia timu yake hiyo ikipoteza mchezo dhidi ya Al Shabab kwa mabao 2-0 katika Ligi Kuu ya UAE wakati wake na marafiki wa kike wa wachezaji wakilazimika kuzindikizwa kutoka nje ya Uwanja wa Al Mamzar, Dubai. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na luninga moja maarfu nchini humo ya Gulf ilisema kuwa vurugu hizo zilianza wakati mshambuliaji wa Mbrazil wa Al Shabab aitwae Ciel ambaye alifunga mojawapo ya mabao ya timu yake mashabiki wa Al Wasl. Mashabiki wa Al Shabab nao wakajibu mapigo kwa kumgeukia rafiki yake wa kike Maradona na aitwae Veronica Ojeda na kuanza kumtupia maneno ya kumdhalilisha. Akihojiwa mara baada ya tukio Maradona amesema kuwa kitendo hicho kimemsononesha sana kwakuwa hakutegemea mashabiki hao wangekuwa waoga kiasi hadi kupelekea kuwashambulia wanawake badala ya kumshambulia yeye mwenyewe.

No comments:

Post a Comment