Wednesday, March 28, 2012

MANCHESTER UNITED ENJOY REFEREEING 'ADVANTAGE' - VIERA.

MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa ambaye kwasasa ni mmoja wa maofisa wa klabu ya Manchester City, Patrick Viera amesema kuwa wapinzani wao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza Manchester United wanasaidiwa na makosa ya waamuzi. Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku mbili baada ya timu ya Fulham kukataliwa penati katika dakika za mwisho katika mchezo baina ya United na timu hiyo uliochezwa katika Uwanja wa Old Trafford ambapo wenyeji waliibuka na ushindi wa bao 1-0. Matokeo hayo yanaifanya United kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama tatu zaidi ya wapinzani wao City. Akihojiwa Viera amesema kuwa United wakati wanacheza nyumbani wanapata faida kama hizo ambazo timu zingine hazipati na sio United pekee hata ukicheza na Real Madrid, Barcelona au AC Milan matatizo kama hayo huwa yanatokea. Aliendelea kusema kuwa faida kama hizo huwa zinapata timu ambazo zimezoea kupata ushindi mara zote hivyo na wao wanahitaji kushinda michezo mingi zaidi ili waweze kupata faida kama hizo huko mbeleni. Wakiwa wamebakisha michezo nane, City wamejikuta wakiwa nyuma ya United kwa alama tatu lakini Viera ambaye amechukua nafasi kama Ofisa wa Maendeleo wa klabu hiyo baada ya kustaafu kucheza anaamini kuwa City wanastahili kuwa mabingwa.

No comments:

Post a Comment