Wednesday, March 28, 2012

SHEIKH KHALIFA WA UAE AMWAGA MINOTI KWA VIJANA WAKE.

RAIS wa Falme za Kiarabu-UAE Sheikh Khalifa bin Zayed ameipa timu ya taifa ya nchi hiyo ya vijana chini ya miaka 23 ambao wamefanikiwa kufuzu michuano ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika jijini London mwaka huu euro 100,000 kila mmoja. Timu hiyo imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya mpira ya nchi hiyo kwa kuifunga Uzbekistan kwa mabao 3-2 mapema mwezi huu. Hayo ni mafanikio makubwa kabisa katika historia ya soka ya nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta toka timu ya wakubwa ya nchi hiyo ilipofanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1990 kwa mara ya kwanza. Sheikh Khalifa aliwapokea wachezaji wa timu hiyo pamoja na viongozi wao katika kasri lake la Dhiyafa lililopo Abu Dhabi mapema wiki hii kabla ya kuwakabidhi zawadi hiyo.

No comments:

Post a Comment