Wednesday, March 28, 2012

KOREA KUSINI KUJIPIMA NGUVU NA HISPANIA.

CHAMA cha Soka cha Korea Kusini-KFA kimetangaza mkakati wake wa kupambana na mabingwa wa dunia Hispania Mei 30 mwaka huu. Timu ya taifa ya Korea inajipanga kumaliza mzunguko wake wa mwisho wa mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 mwezi Juni mwaka huu hivyo mchezo huo utakuwa mahsusi kwa ajili ya maandalizi ya michezo hiyo. Korea ambao wanajulikana kwa jina la utani la Taeguk Warriors wako katika kundi A wakiwa na timu za Iran, Uzbekistan, Qatar na Lebanon ambapo wanatarajia kucheza mchezo wao wa mzunguko wa nne jijini Doha Juni 8 mwaka huu. Kwa upande wa Hispania wao watatumia mchezo huo kama maandalizi ya michuano ya Ulaya ambayo inatarajiwa kuchezwa Juni mwaka huu huko Poland na Ukraine ambapo mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo wamepangwa kundi C wakiwa na timu za Italia, Jamhuri ya Ireland na Croatia.

No comments:

Post a Comment