Wednesday, March 28, 2012

HEART SPECIALIST: MUAMBA UNLIKELY TO RETURN.

BAADA ya moyo kushindwa kufanya kazi wakati wa mchezo wa Kombe la FA kati ya Bolton Wanderers na Tottenham Hotspurs katikati ya mwezi huu Fabrice Muamba hatarajiwi kucheza soka tena kwa mujibu wa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo. Mkurugenzi mtabibu wa Mfuko wa Magonjwa ya Moyo Peter Weissberg amekiri kuwa itakuwa sio suala sahihi kwa mtu kumshauri mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza ya vijana chini ya miaka 21 kuendelea kucheza soka. Weissberg anaelewa kuwa suala la Muamba kucheza soka tena sio rahisi kwa sababu tatizo la kusimama kwa moyo wake kufanya kazi limechangiwa kwa kiasi kikubwa na na mazoezi anayofanya hivyo itakuwa sio busara mchezaji huyo kurejea uwanjani tena. Akihojiwa Weissberg amesema kuwa sio rahisi kusema kwasasa lakini anafikiri mchezaji atashauriwa kutocheza soka tena kwasababu tatizo hilo lililomkumba linachangiwa kwa kiasi kikubwa na mazoezi magumu anayofanya. Tatizo la moyo kwa wachezaji mpira limekuwa ni la kawaida kutokana na matukio mengi kuwa yanatokea katika miaka ya hivi karibuni wakiwemo wachezaji kama Ruben de la Red na Sergio Sanchez kupumzika kucheza kutokana na matatizo hayo wakati Marc Vivien Foe, Antonio Puerta na Dani Jargue wote walikufa kutokana na matatizo ya moyo.

No comments:

Post a Comment