Thursday, March 22, 2012

MANCINI AFUNGUKA KUHUSU TEVEZ.

KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini anatarajia Carlos Tevez atasaidia sana klabu yake kutimiza ndoto za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kuanza kazi rasmi jana. Tevez alikuwa kivutio kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Chelsea akirejea kwa mara ya kwanza tangu Septemba usiku wa jana Uwanja wa Eastlands, ingawa alianzia benchi. Mshambuliaji huyo wa Argentina alitengeneza bao la ushindi lilifungwa na Samir Nasri na kuifanya timu yake ipunguze pengo la pointi hadi kubaki moja dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Manchester United. Sergio Aguero alisawazisha kwa penalti dakika chache tu baada ya Tevez kuingia hivyo kufanya mchezo uwe 1-1 baada ya Gary Cahill kutangulia kuifungia Chelsea. Akihojiwa mara baada a mchezo huo Mancini amesema kuwa Carlos alifanya vizuri kutoa pasi ya mwisho ambayo Nasri alifunga na mashabiki walifurahia hilo ila mchezaji huyo anahitaji muda zaidi na haitakuwa kazi rahisi lakini pengine baada ya muda wa wiki mbili huko mbele atakuwa katika kiwango kizuri zaidi.

No comments:

Post a Comment