Thursday, March 22, 2012

STEVANOVIC KUIBURUZA GHANA FA FIFA.

BAADA ya kutimuliwa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana aliyekuwa kocha wa timu hiyo Goran Stevanovic amelitahadharisha Shirikisho la Soka la Ghana-GFA kuhusu malipo yake mara baada ya kuvunja mkataba wake. Kocha huyo raia wa Serbia amewapa siku 14 mabosi wake hao kumlipa fedha zake zote na kama wakishindwa kufanya hivyo basi atawashitaki GFA kwa Shirikisho la Soka duniani-FIFA. Katika barua hiyo iliyotumwa kwa GFA imeweka wazi kuwa hakubaliani na ombi la shrikisho hilo kumlipa mshahara wa miezi mitatu na badala yake wanahitaji mshahara wote wa miezi 24 kama walivyokubaliana wakati anasaini mkataba. Barua hiyo iliendelea kusema kuwa kama GFA haitatimiza hilo suala ndani ya siku 14 basi watalipeleka suala hilo ikaamuliwe FIFA. Jumatatu iliyopita Stevanovic alitimuliwa kibarua cha kukinoa kikosi hicho ambacho alianza kukifundisha Januari mwaka 2011 ambapo alikuwa akilipwa kiasi cha euro 30,000 kwa mwezi na nafasi yake imechukuliwa na msaidizi wake Kwesi Appiah ambaye atakaimu nafasi hiyo mpaka atakapopatikana kocha wakudumu.

No comments:

Post a Comment