Friday, March 23, 2012

WENGER WANT QUALITY NOT QUANTITY.

KOCHA wa Arsenal amewaonya mashabiki wa timu hiyo kuwa wasitegemee mabadiliko makubwa katika klabu yake mwishoni mwa msimu huu kwasababu amepanga kununua wachezaji wenye majina makubwa. Mashabiki klabu hiyo wamekuwa na hasira na kocha huyo kutokana na kushindwa kusajili wachezaji ambao watakata kiu ya timu hiyo kukosa vikombe kwa miaka saba sasa nab ado wamendelea kumhimiza kutafuta wachezaji wazuri msimu ujao. Lakini Wenger ambaye Ijumaa alikataa taarifa kwamba mshambuliaji wa kimataifa kutoka Ujerumani Lukas Podolski amefanyia vipimo vya afya katika harakati za kujiunga na klabu hiyo ameamua kusajili wachezaji ambao anaamini kuwa watakuwa na kipaji kulingana fungu atakalokuwa nalo. Akihojiwa Wenger amesema kuwa kwasasa wana idadi ya wachezaji 25 huku wengine wengi wakiwa wancheza kwa mkopo katika klabu zingine na pia wamecheza bila Jack Wilshere na Abou Diaby karibu msimu mzima kutoka majeraha waliyonayo ambapo kama wachezaji hao wakirudi na kikosi kitaimarika zaidi kwani hata sasa wako katika nafasi nzuri bila kuwa na hao wachezaji. Kwasasa kocha huyo anakiwa kuhakikisha timu hiyo inamaliza ikiwa juu ya Tottenham Hotspurs na Chelsea katika nafasi ya tatu mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza ili kujihakikishia nafasi ya moja kwa moja kushiriki michuano ya Klabu Bingwa ya Ulaya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment