Wednesday, May 9, 2012
BAADA YA IRAQ KUCHOMOA, IRAN SASA KUCHEZA NA ALBANIA.
SHIRIKISHO la Soka la Iran limesema kuwa timu ya taifa ya nchi hiyo itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na Albania baada ya mchezo baina yake na Iraq uliokuwa uchezwe Mei 27 kufutwa. Shirikisho la Soka la Albania-FSHF lilithibitisha taarifa hizo kupitia katika mtandao wake huku kukiwa na menelezo kuwa mchezo huo utachezwa Mei 27 hukohuko jijini Istanbul, Uturuki. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na gazeti la Tehran Times Iraq ilifuta mchezo huo kutokana na kutofikia makubaliano na Iran juu ya wapi mchezo huo uchezwe. Iran inatarajiwa kuanza kambi yake Mei 21 na itatumia mchezo huo wa kirafiki ili kujiweka sawa na mchezo wao wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Uzbekistan Juni 3 mwaka huu. Albania ambao walishindwa kufuzu michuano ya Ulaya inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao ambapo kwasasa wanashika nafasi ya 84 katika orodha za ubora duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment