Jana, Katibu wa Baraza la Wazee la klabu, Ibrahim Ally Akilimali alisema kipigo cha 5-0 kimetokana na wachezaji kutokuwa na morali kwa sababu wanaidai fedha nyingi klabu. “Hakuna anayedai, wote tulilipwa madai yetu kabla ya mechi, tena yote,”alisema Tegete. Kwa sasa Yanga kuna mgogoro unaosababishwa na wazee wa klabu hiyo, ambao wanampiga vita Mwenyekiti wa klabu hiyo, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga wakitaka aondoke madarakani.
Inadaiwa wazee hao wanatumiwa na kiongozi mmoja wa zamani wa Yanga, ambaye nia yake awe yeye bosi wa klabu. Inadaiwa hata kipigo cha 5-0, kilitokana na wapinzani hao wa Nchunga kuwahonga baadhi ya wachezaji wacheze chini ya kiwango. Na kauli yao ya kusema wachezaji hawana morali ndio maana walifungwa, ilifuatia Nchunga kusema kuna wachezaji walihujumu timu na watafukuzwa.Walichokifanya wazee hao, walikuwa kama wanawatetea wachezaji wasifukuzwe- wakati kihistoria klabu ilikwishawahi kufukuza wachezaji baada ya kufungwa 4-1 na Simba mwaka 1994.
STORY BIN ZUBERY.
No comments:
Post a Comment