Wednesday, May 9, 2012

PUYOL KUKOSA EURO 2012.

BEKI wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona Carles Puyol anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mguu na kupelekea kuwa nje wakati timu ya taifa ya nchi hiyo ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano ya Kombe la Ulaya itakapokuwa ikitetea taji lake. Puyol alikuwa akijisikia maumivu katika mguu wake wa kulia wa timu yake ya Barcelona ilipoibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Espanyol Jumamosi iliyopita na baada ya kufanyiwa vipimo ilionekana kuwa mchezaji huyo anahitaji kufanyiwa upasuaji ili kutibu tatizo hilo. Mchezaji huyo alikosa sehemu kubwa ya michezo ya mwishoni mwa ligi msimu uliopita baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wa kushoto lakini alipona vyema na kucheza msimu huu wote. Puyol ameichezea Hispania michezo 99 na amekuwa sehemu ya kikosi hicho ambacho kimeshiriki michuano yote mikubwa ya dunia toka mwaka 2002.

No comments:

Post a Comment