FIFA, BRAZIL WAMALIZA TOFAUTI ZAO.
|
Jack Valcke |
VIONGOZI wa soka Brazil na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA wamemaliza tofauti zao zilizojitokeza hivi karibuni na sasa wanashirikiana kwa nguvu zote kuhakikisha maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 yanakuwa yamafanikio. Mkutano uliokaribia kuchukua saa sita ambao ni wa kwanza kati ya Waziri wa Michezo wa nchi hiyo Aldo Rebelo na Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valcke toka katibu huyo alipotoa kauli kuhusiana na maandalizi ya taratibu yanayofanywa na nchi hiyo mapema mwaka huu. Kauli aliyoitoa Valcke ilipingwa na serikali ya nchi hiyo ambapo Rebelo alitoa kauli ya kutoshirikiana na katibu huyo kwa jambo lolote katika maandalizi hayo kwa kauli yake hiyo ambayo alidai ni ya kuudhi na kudhalilisha. Mara baada ya mkutano huo FIFA ilitangaza kuwa mjumbe mmoja kutoka serikali ataungana na Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Dunia ili kurahisisha mawasiliano kati ya serikali na kamati hiyo kwenye maandalizi hayo.
No comments:
Post a Comment