Wednesday, May 9, 2012
MCHEZAJI WA JAMHURI YA IRELAND ATISHIWA KUUWAWA.
MCHEZAJI wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland, James McClean ametishiwa kuuwawa baada ya kujumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kinachonolewa na kocha Giovanni Trappatoni ambacho kitashiriki michuano ya Ulaya itakayofanyika mwezi ujao. Vitisho vya kuuliwa vimekuja kufuatia mchezaji huyo kuichezea timu ya vijana chini ya miaka 21 ya Ireland ya Kaskazini ambao wako chini ya Uingereza halafu kubadilisha na kuamua kuichezea timu ya wakubwa ya Jamhuri ya Ireland ambalo ni taifa linalojitegemea. McClean ambaye ana miaka 23 ambaye anacheza katika klabu ya Sunderland alijumuishwa katika kikosi cha Trappatoni ambacho kilitangazwa jana. Akionyesha furaha ya kuchaguliwa katika kikosi hicho McClean aliandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kufurahishwa na uteuzi huo na kusema kuwa atahakikisha anafanya kila liwezekanalo ili timu yake iweze kupata mafanikio katika michuano hiyo. Mara baada ya kutuma ujumbe huo alianza kupokea ujumbe wa vitisho vya kuuwawa kitendo kilichopelekea kufunga mtandao wake huo wa kijamii, ambapo hivi sasa polisi wanafanyia uchunguzi tukio hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment