Monday, August 20, 2012

ARSENAL YAKARIBIA KUMCHUKUA SAHIN KWA MKOPO.

KLABU ya Arsenal inakaribia kumpata kwa mkopo kiungo wa klabu ya Real Madrid Nuri Sahin ili kuziba pengo la Alex Song ambaye amesajiliwa na Barcelona. Sahin mwenye umri wa miaka 23 ambaye pia alikuwa akiwindwa na klabu ya Liverpool katika kipindi hiki usajili anatarajiwa kujiunga na Arsenal kwa msimu mzima wa Ligi Kuu huku kukiwa na uwezekano wa kumchukua moja kwa moja. Klabu hiyo inatarajiwa kutangaza ujio wa mchezaji huyo ambaye ni raia wa Uturuki baadae wiki hii ili kuziba pengo la Song ambaye amekwenda Barcelona kwa uhamisho wa paundi milioni 15. Sahin ambaye alijiunga na mabingwa hao wa Hispania akitokea klabu ya Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka sita aliosaini Mei mwaka 2011 ameshindwa kuonyesha cheche kutokana na majeraha ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakimwandama. Meneja wa Liverpool Brandan Rodgers ambaye amewahi kufanya kazi chini ya kocha wa Real Madrid Jose mourinho wakati akiinoa Chelsea naye alikuwa na matumaini ya kumpata Sahin ili kuongeza nguvu katika kikosi chake.

No comments:

Post a Comment