Monday, August 20, 2012

PEPE ALAZWA.

BEKI wa klabu ya Real Madrid, Pepe amelazwa hospitali kwa uchunguzi baada ya kuumia kichwa kwa kugongana wakati wa mchezo baina ya timu hiyo na Valencia ambao walitoka sare ya bao 1-1 jana. Pepe aligongana na mchezaji mwenzake Iker Casillas katika dakika ya 42 ya mchezo huo wakati wakijaribu kuokoa mpira wa kona uliopigwa katika lango lao na kuzaa bao la Valencia. Wachezaji wote wawili waliendelea na mchezo kama kawaida kabla ya Pepe kubadilishana na Raul Albiol katika kipindi mapumziko na kupelekwa moja kwa moja hospitali kwa uchunguzi. Klabu imesema katika mtandao wake kuwa baada ya kufanyiwa vipimo havikuonyesha kupata tatizo lolote katika ubongo lakini itabidi abakie hospitalini hapo kwa masaa mengine 24 ili wajiridhishe.

No comments:

Post a Comment