KIUNGO wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana, Quinton Fortune aliwashangaza wapenzi wa Manchester United wakati alipovaa jezi ya timu hiyo na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Aberdeen ya Scotland jana usiku. Fortune aliondoka United mwaka 2006 lakini ameendelea kuwa karibu na timu hiyo akiwa kama balozi wake. Mbali ya Fortune katika mchezo huo pia walikuwemo wachezaji wengine wa sasa wa klabu hiyo kama David de Gea, Rio Ferdinand, Paul Scholes, Anderson, Bebe, Ryan Giggs na Darren Fletcher ambaye alirejea dimbani baada ya kutocheza kwa muda mrefu kutokana na majeruhi. Mchezo huo ulikuwa wa hisani lakini msimu mpya wa Ligi Kuu ya uingereza unakaribia kuanza siku chache zijazo hivyo pia ulikuwa muhimu kwa baadhi ya wachezaji wa United. Aberdeen ilishinda mchezo huo kwa mabao 2-1 ambapo Fortune alikosa nafasi ya wazi ya kusawazisha bao katika dakika za mwisho baadaya kuingia akitokea katika benchi la wachezaji wa akiba katika dakika ya 68. Fortune ameichezea United michezo 76 katika misimu saba ambayo amekuwa na klabu hiyo akicheza katika nafasi ya kiungo pamoja na beki wa kushoto.
No comments:
Post a Comment