Tuesday, August 14, 2012

LIBYA-ALGERIA KUCHEZA MOROCCO.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limeiruhusu Libya kucheza mchezo wake wa nyumbani wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika 2013 dhidi ya Algeria jijini Casablanca, Morrocco Septemba 9 mwaka huu. Mashirikisho ya nchi zote mbili wamekubaliana na mabadiliko hayo ambapo mara ya kwanza mchezo huo ulikuwa umepangwa kuchezwa jijini Tripoli lakini kutokana na hali ya kiusalama kutotengemaa katika mji huo ndio maana ukahamishwa kupelekwa Algeria. Mapema kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic alifuta ratiba ya kucheza mchezo wa kirafiki uliokuwa uchezwe Agosti 15 na badala yake atatumia muda huo kuwapa semina wachezaji wa timu hiyo kwenye kituo cha ufundi ch kitaifa kilichopo Sidi Moussa karibu na jiji la Algiers. Libya nao wanatarajiwa kufanya semina kama hiyo itakayofanyika jijini Tripoli, wakati mchezo wao mwingine wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 dhidi Cameroon utafanyika jijini Sfax, Tunisia.

No comments:

Post a Comment