Tuesday, August 14, 2012

OLYMPICS FLAG ARRIVES AT RIO DE JANEIRO.

OLYMPIC FLAG.
BENDERA rasmi ya michuano ya Olimpiki imewasili katika jiji la Rio de Janeiro nchini Brazil, mji ambao ndio utakuwa mwenyeji wa michuano hiyo inayofuata. Meya wa jiji hilo Eduardo Paes alikabidhiwa bendera hiyo jijini London, Uingereza kabla ya kuzimwa kwa mwenge wa olimpiki ikiwa kama alama ya kuanza kwa maandalizi ya michuano hiyo jijini Rio de Janeiro mwaka 2016.
Paes aliwasili na bendera hiyo ya olimpiki akiongozana na rais wa Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo mwaka 2016, Gavana wa Rio de Janeiro Sergio Cabral pamoja na wanariadha wan chi hiyo walioshiriki katika michuano ya jijini London. Brazil walimaliza michuano hiyo wakiwa katika nafasi ya 22 wakiwa wamejikusanyia medali 17, mbili zaidi ya walizopata katika michuano hiyo iliyofanyika jijini Beijing mwaka 2008. Rio de Janeiro ndio mji wa kwanza wa Amerika Kusini kuwa wenyeji wa michuano ya olimpiki, ingawa kumekuwa na wasiwasi juu ya maandalizi kukamilika kwa wakati kutokana na ujenzi wa viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo kuchelewa kuanza.

No comments:

Post a Comment