PETROV AENDELEA VYEMA NA MATIBABU YA LEUKAEMIA.
|
Stiliyan Petrov. |
KLABU ya Aston Villa imebainisha kuwa nahodha wake Stiliyan Petrov yuko mbioni kupona ugonjwa wa kansa ya damu au Leukaemia unamkabili. Kiungo huyo wa kimataifa wa Bulgaria aligundulika na ugonjwa huo mwezi uliopita na amekuwa akipatiwa matibabu ili kudhibiti ugonjwa huo na klabu hiyo imethibitisha katika taarifa yake kuwa anaendelea vyema. Taarifa ya klabu hiyo iliendelea kusema kuwa kiungo huyo anatoa shukrani za dhati kwa madaktari ambao wanamshughulikia toka agundulike na ugonjwa huo kwa kumhudumia vyema. Petrov pia ameashukuru ashabiki wa klabu hiyo, wachezaji wenzake pamoja na wapenzi wote wa soka duniani kwa kumuunga mkono katika kipindi hicho kigumu kinachomkabili.
No comments:
Post a Comment