MENEJA wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini amemjia juu na kumponda golikipa wake Joe Hart baada ya Cristiano Ronaldo kuifungia bao la ushindi Real Madrid katika dakika za majeruhi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Hart alionyeshwa kuchukizwa na kitendo cha timu yake kuwa mbele kwa mabao 2-1 zikiwa zimebakia dakika tatu mchezo kumalizika kabla ya Madrid kusawazisha na kuongeza la ushindi na kupelekea timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-2. Lakini Mancini alimjia juu golikipa huyo na kumwambia kuwa hana haki ya kulaumu mwenye haki ya kufanya hivyo ni yeye mwenyewe kwani alichotakiwa kufanya hart na kukaa golini na kujaribu kuokoa hatari zilizokuwa zikiwakabili katika dakika hizo za mwisho. Mancini alikiri kuwa hivi sasa msukumo umekuwa mkubwa katika kundi D lakini alisisitiza kuwa hatarajii City kuenguliwa tena katika hatua ya makundi msimu huu. Michuano hiyo inaendelea tena leo ambapo Chelsea watakuwa wenyeji wa Juventus, Manchester United nayo itaikaribisha Galatasaray ya Uturuki huku Bayern Munich nao wakiikaribisha Valencia wakati Barcelona watakuwa wenyeji wa Spartak Moscow. Michezo mingine itazikutanisha timu za Braga ambayo itamenyana na CFR Cluj, Lille itapimana ubavu na BATE, Shaktar Donetsk itapepetana na Nordsjaelland huku Celtic wakichuana na Benfica.
No comments:
Post a Comment