Wednesday, September 19, 2012

MAOFISA FIFA WATUA JAPAN KUKAGUA VIWANJA VYA CLUB WORLD CUP.

MAOFISA wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ambao walipitisha mifumo miwili ya teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli waliwasili nchini Japan jana kwa ajili ya kukagua viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia. Maofisa hao wametua nchini humo ikiwa yamepita masaa machache baada ya timu ya Everton nayo kukataliwa bao la wazi ambapo mpira ulionekana kuvuka mstari lakini mshika kibendera alishindwa kuona sawasawa na kukataa bao hilo katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Newcastle. Ligi Kuu ya nchini Uingereza ilikuwa ya kwanza kutaka kutumia mojawapo ya mifumo hiyo lakini walishindwa kufanya hivyo baada ya muda kutoruhusu kufanya hivyo. Mifumo hiyo ambayo mmoja unaitwa Hawk-Eye na GoalRef inatarajiwa kuwekwa katika viwanja viwili tofauti kila mmoja nchini Japan kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia hayo yakiwa majaribio yake ya mwisho kabla ya kuanza kutumika ramsi katika mashidano mbalimbali.


No comments:

Post a Comment