Tuesday, September 18, 2012

MOYES ALALAMIKIA MABAO WALIYOKATALIWA.

Moja ya bao lililokataliwa likionekana kuvuka mstari.
MENEJA wa klabu ya Everton David Moyes amemlalamikia mwamuzi msaidizi Ceri Richards aliyechezesha mchezo baina ya timu yake na Newcastle ambao uliisha kwa sare ya mabao 2-2 kwa kuinyima timu yake mabao mawili ya wazi. Mwamuzi huyo alinyoosha kibendera kimakosa akidhani Marouane Fellaini alikuwa ameotea wakati akifunga bao kipindi cha pili kabla ya kushindwa kuona mpira uliokuwa umevuka mstari wa goli uliopigwa kwa kichwa na Victor Anichebe. Moyes alikiri kuwa mara baada ya mchezo huo alienda katika vyumba vya waamuzi lakini sio kwa ugomvi bali kumwambia mshika kibendera huyo kama aliyaona mabao hayo mawili aliyokataa. Meneja wa Newcastle nae alikiri kuwa mshika kibendera huyo alifanya makosa kwani mpira aliopiga Anichebe ulikuwa kweli umevuka mstari na kusema kuwa kuna umuhimu wa mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli kuanza kutumika.

No comments:

Post a Comment