Tuesday, September 18, 2012

WENGER KUANZIA JUKWAANI UFARANSA.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anatarajiwa kukaa jukwaani na kumuangalia msadizi wake Steve Bold akichukua nafasi yake wakati klabu hiyo itapopambana na Montpellier katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baadae leo. Wenger hatakuwemo kwenye benchi la ufundi kutokana na kuanza adhabu yake ya kufungiwa michezo mitatu na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA hivyo majukumu inabidi amuechie msaidizi wake huyo. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Wenger amesema kuwa anamwamini Bould kwakuwa amekuwa akifanya kazi yake vyema na huko mbele atakuaja kuwa kocha mzuri kwasababu vigezo anavyo. UEFA ilimfungia Wenger baada ya kumkashifu mwamuzi Damir Skomina wakati wakielekea katika vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya AC Milan msimu uliopita. Wenger anatakiwa kuitumikia adhabu hiyo ndani ya miezi 12 wakati michuano hiyo itakapokuwa ikiendelea.

No comments:

Post a Comment