Monday, October 22, 2012

KABLA YA KUJA URUSI NILITAKA KUJIUNGA NA PSG - ETO'O.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi, Samuel Eto’o ameweka wazi kuwa aliwahi kufanya mazungumzo na klabu ya Paris Saint-German-PSG katika kipindi cha majira ya kiangazi. Eto’o mwenye umri wa miaka 31 ambaye alihamia klabu hiyo tajiri nchini Urusi msimu uliopita akitokea Inter Milan kwa ada ambayo inaaminika kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani. Mshambuliaji huyo kimataifa wa Cameroon amekiri kuwa kabla ya kwenda nchini Urusi alikaribia kujiunga PSG lakini hawakufikia muafaka katika mazungumzo yao na kuamua kumfuata Zlatan Ibrahimovic. Pamoja na mazungumzo aliyofanya na PSG Eto’o ambaye amewahi pia kcheza katika klabu ya Barcelona amesisitiza ana furaha kuwepo nchini Urusi katika klabu hiyo wakati pia anajipanga kuisaidia timu yake ya taifa katika michezo yake ya kimataifa baada ya kuerejea tena kwenye timu hiyo.

No comments:

Post a Comment