Monday, October 22, 2012

NI NGUMU UBAGUZI KUTOKOMEZWA MOJA KWA MOJA.

MENEJA wa klabu ya Queens Park Rangers-QPR, Mark Hughes ameonya kuwa itakuwa ni suala lisilowezekana moja kwa moja kuondoa tatizo la ubaguzi wa rangi michezoni. Zaidi ya wachezaji 30 kutoka vilabu nane vya Ligi Kuu ya nchini Uingereza walioamua kutovaa fulana za Kick It Out mwishoni mwa wiki fulana ambazo ni mahsusi kwa ajili ya kampeni za kupinga ubaguzi michezoni. Mmoja wapo ya wachezaji ambao hawakuvaa fulana hizo ni pamoja na beki wa QPR Anton Ferdinand ambaye alikumbwa na tatizo la kubaguliwa na nahodha wa Chelsea John Terry msimu uliopita. Hughes amesema kuwa ni vigumu kulitokomeza tatizo la ubaguzi moja kwa moja kama jitihada za makusudi kama kuongeza adhabu kwa watu wanaofanya vitendo hivyo hazitachukuliwa ili kulipa kipaumbele suala hilo. Ferdinand aliungana na wachezaji wenzake Djibril Cisse, Shaun Wright-Phillips, Nedum Onouha na Junior Hoilett kutovaa fulana hizo ili kushinikiza hata kali zaidi zichukuliwe kwa watu wenye vitendo vya kibaguzi.

No comments:

Post a Comment