Monday, October 22, 2012

VENUS WILLIAMS AKATA KIU YA MATAJI.

MCHEZA tenisi nyota kutoka Marekani, mwanadada Venus Williams amekata kiu ya miaka miwili ya kutoshinda taji lolote baada ya kunyakuwa taji la michuano ya wazi ya Luxembourg likiwa ni taji la 44 toka aanze kucheza tenisi. Williams mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikuwa anacheza fainali yake ya 71 toka aanze kucheza mchezo huo alifanikiwa kumfunga Monica Niculescu mwenye umri wa miaka 25 kutoka Romania kwa seti 2-0 zenye alama za 6-2 6-3. Williams ni mmoja wapo ya wachezaji ambao bado wanacheza mchezo huo wenye mataji mengi zaidi akitanguliwa na mdogo wake Serena ambaye ana mataji 45 na ana anafasi ya kuongeza taji lingine katika michuano ya WTA inayotarajiwa kufanyika jijini Istanbul baadae wiki hii. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Venus amesema kuwa alifanya jitihada kubwa kuhakikisha anafika fainali katika michuano hiyo na anamshukuru mungu azma yake imefanikiwa na anatgemea kufanya vizuri zaidi kabla hajaamua kustaafu mchezo huo. Mara ya mwisho Williams kushinda taji ilikuwa ni katika michuano ya Acapulco Februari mwaka 2010 ambapo baada ya hapo kiwango chake kikaporomoka.

No comments:

Post a Comment