Thursday, October 11, 2012

MTANANGE WA AL AHLY NA SUNSHINE STARS KUPIGWA BILA MASHABIKI.

MCHEZO wa nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kati Al Ahly ya Misri na Sunshine Stars ya Nigeria ambao utachezwa jijini Alexandria au Cairo unatarajiwa kuchezwa katika uwanja mtupu. Katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo ambayo ilitumwa kwa Chama cha Soka imefafanua kuwa hawataweza kuwahakikishia usalama mashabiki watakaohudhuria mchezo huo ambao unaweza kuchezwa katika Uwanja wa Jeshi uliopo jijini Cairo au Uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria Octoba 21 mwaka huu. Kutokana na suala hilo la usalama kutokuwa wa uhakika ndio wamefikia uamuzi wa kuwataarifu Al Ahly kucheza mchezo wao huo dhidi ya Sunshine bila ya mashabiki kuwepo uwanjani. Serikali nchini Misri ilifungia viwanja vyote kutokuwepo mashabiki wakati wa mechi kufuatia ghasia zilizotokea Port Said ambazo zilizopelekea vifo vya watu zaidi ya 70 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya nchi hiyo kati ya Al Ahly na Al Masry.

No comments:

Post a Comment