Friday, October 26, 2012

NITASHIKANA MIKONO NA TERRY - ROBERTS.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Reading Jason Roberts amesema kuwa atashikana mikono na John Terry lakini amekataa kuweka wazi kama anafikiri nahodha huyo wa Chelsea ni mbaguzi. Terry ambaye ni nahodha wa zamani wa Uingereza amefungiwa mechi nne na kutozwa faini ya paundi 220,000 baada ya kukutwa na hati ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi Anton Ferdinand wa Queens Park Rangers mwaka jana. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Roberts amesema kuwa atashikana mikono na Terry lakini alipoulizwa kama anadhani beki huyo ni mbaguzi alikwepa swali hilo na kurudia sentensi yake ya kwanza. Ikiwa ni mwaka mmoja umepita toka kutokea kwa tukio hilo la Terry lakini kumekuwa na muendelezo wa matukio ya aina hiyo sehemu tofauti likiwemo tukio la mwezi ambapo beki wa timu ya vijana wa miaka chini ya 21 ya Uingereza Danny Rose alianyiwa vitendo vya kibaguzi wakati wa mechi nchini Serbia. Roberts aliungana na wachezaji wengine weusi nchini Uingereza wakiwemo Rio na Anton Ferdinand kutovaa tisheti za kampeni ya kutokomeza ubaguzi michezoni wakidai kusuasua kwa juhudi za kupiga vita suala hilo.

No comments:

Post a Comment