Friday, October 26, 2012

VETTEL AJITENGENEZEA NAFASI NZUR YA KUNYAKUWA TAJI LA INDIAN GRAND PRIX.

DEREVA nyota wa mbio za magari za Langalanga, Sebastian Vettel amefanikiwa kupata nafasi ya kwanza kabla ya kuanza kwa michuano ya Indian Grand Prix nafasi ambayo imemuweka katika nafasi nzuri ya kushinda mashindano hayo kwa mara ya nne mfululizo Jumapili. Vettel mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ujerumani kutoka timu ya Redbull ambaye anaongoza orodha ya madereva bora kwa alama sita zaidi ya Fernando Alonso wa timu ya Ferrari alitumia muda mzuri wa dakika moja na sekunde 27. Dereva wa timu ya MacLaren Jenson Button alishika nafasi ya pili katika mbio hizo huku Alonso akikamata nafasi ya tatu na nafasi ya nne kwenda kwa Lewis Hamilton wakati tano bora ilifungwa na dereva mwenzake Vettel wa timu ya Redbull Mark Webber. Mashindano hayo yatafanyika ramsi Jumapili huku Vettel akipambana vilivyo kuhakikisha anashinda na kujiongezea alama ili aweze kuwa bingwa wa dunia mwishoni mwa msimu huu ambao kumebakiwa na mshindano manne pekee.

No comments:

Post a Comment