Thursday, October 25, 2012

TANZIA NGUMI.

KOCHA Emanuel Steward ambaye amewafundisha mabondia nguli kama Thomas Hearns, Lennox Lewis na Wladimir Klitschko amefariki dunia akiwa na miaka 68. Alianza kujizolea umaarufu wakati alipokuwa akifundisha jijini Detroit ambapo Hearns aliyekuwa mwanafunzi wake alipokuwa bingwa wa dunia mwaka 1980. Steward ambaye ni raia wa Marekani ndio bondia aliyefundisha mabondia wengi zaidi ambao ni mabingwa wa dunia kuliko kocha yoyote wa mchezo huo na alifanya kazi na bingwa wa uzito wa juu Klitschko Julai mwaka huu. Klitschko alituma salamu zake za rambirambi kwa Steward akimuelezea kama mwalimu bora wa mchezo huo kupata kutokea na kwamba ulimwengu wa masumbwi umempoteza mtu muhimu. Steward ambaye alikuwa akisumbuliwa na kansa ya utumbo pia aliwafundisha mabondia wakubwa kama Wilfred Benitez, Julio Cesar Chavez, Oscar de la Hoya, Evander Holyfield, Mike McCallum na James Toney. 

No comments:

Post a Comment