Thursday, October 25, 2012

SEREA AMGARAGAZA TENA AZARENKA.

MCHEZAJI nyota anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake mwanadada Victoria Azarenka amebakia katika mashaka kama atamaliza mwaka huu katika nafasi hiyo baada ya kufungwa na Serena Williams kwa mara ya tano katika vipindi tifauti walivyokutana mwaka huu. Azarenka ambaye anatoka Belarus alikubali kufungwa kwa 6-4 6-4 naWilliams kutoka Marekani katika michuano ya WTA inayofanyika jijini Istabul ambapo sasa itabidi ahakikishe anamfunga Li Na bingwa wa zamani wa michuano ya wazi ya Ufaransa kutoka China ili aweze kujihakikishia nafasi hiyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Williams amesema kuwa alifanya mazoezi ya nguvu ili aweze kucheza vyema na anatarajia ataendlea kufanya vyema na kama ikishindikana atajaribu kufanya hivyo tena mwakani. Azarenka ambaye alifungwa na Williams katika michuano ya wazi ya Marekani mwezi uliopita alianza vyema mchezo huo kwa kuongoza katika seti ya kwanza lakini Williams ambaye naye alikuwa akicheza chini ya kiwango alikuja juu na kuhakikisha hapotezi mchezo huo muhimu.

No comments:

Post a Comment