Friday, October 26, 2012

RATIBA YA NAKUNDI ULAYA YASOGEZWA MBELE.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limeamua kusogeza mbele upangwaji wa ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Europa League hatua ya mtoano. Shughuli hiyo kwa kawaida ilitakiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu lakini wamesogeza mbele kwa siku sita zaidi kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi. Katika taarifa ya UEFA iliyotumwa katika mtandao imesema kuwa ratiba ya hatua ya mtoano ya michuano hiyo ya Ulaya 2012-2013 ambayo kwa kawaida hufanyika Desemba 14 sasa imesogezwa mbele mpaka Alhamisi Desemba 20 katika makao makuu ya shirikisho hilo jijini Nyon, Switzerland. Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itafanyika katika Uwanja wa Wembley jijino London Uingereza May 25 mwakani huku fainali ya Europa League yenyewe itafanyika jijini Amsterdam, Uholanzi katika Uwanja wa ArenA 10 siku kumi baadae.

No comments:

Post a Comment