Sunday, November 4, 2012
CAF NAME SHOTLIST FOR 2012 AWARDS.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ghana, Andre Ayew ndiye mchezaji pekee wa nchi hiyo kujumuishwa katika orodha ya wachezaji watakaogombea tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka huu. Kiungo huyo alikuwa katika orodha ya wachezaji watatu bora mwaka uliopita sambamba na Yaya Toure ambaye alinyakuwa tuzo hiyo na Seydou Keita wa Mali. Wachezaji wengine waliopo katika orodha hiyo na nchi zao ni pamoja na John Mikel Obi-Nigeria, Alex Song-Cameroon, Christopher Katongo-Zambia, Demba Ba-Senegal, Didier Drogba- Ivory Coast, Gervinho-Ivory Coast, Pirre-Emerick Aubameyang-Gabon, Younes Belhanda-Morocco na Yaya Toure-Ivory Coast. Majina hayo kumi yatapunguzwa na kubakia matatu mwishoni mwa Novemba kabla ya mshindi kutangazwa katika sherehe zitakazofanyika jijini Accra, Ghana Desemba 20 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment