FERGUSON ATANIA KUPIGA PENATI MWENYEWE BAADA YA WACHEZAJI WAKE KUKOSA MARA KWA MARA.
MENEJA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwa utani amependekeza kuwa anaweza kupiga penati mwenyewe siku nyingine baada ya Wayne Rooney kukosa penati wakati timu hiyo ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal Jumamosi. Mabao ya Robin van Persie na Patrice Evra yalitosha kuihakikishia United alama zote tatu na kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingerezakwa mara ya kwanza msimu huu lakini timu hiyo ingeweza kupata mabao zaidi kama Rooney asingekosa penati baada ya Santi Cazorla kuunawa mpira katika eneo la hatari. Rooney anakuwa mchezaji wa`nne wa timu hiyo kukosa penati katika michezo ya hivi karibuni baada ya Van Persie, Javier Hernandez na Nani na kukosa nafasi kama hiyo msimu huu. Ferguson amesema kuwa amsikitishwa na kitendo cha Rooney kukosa penati hiyo lakini suala la msingi lilikuwa ni ushindi kwenye mchezo huo hivyo anashukuru walifanikiwa huku akitania kuwa kama itatokea nafasi nyingine ya kupiga penati katika mchezo mwingine atapiga mwenyewe..
No comments:
Post a Comment