Monday, November 5, 2012

CITY HAIKO TAYARI KUSHINDA CHAMPIONS LEAGUE.

MENEJA wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini amesema kuwa kikosi chake kilichosheheni nyota walionunuliwa kwa pesa nyingi bado hakipo tayari kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kauli yao imekuja kufuatia mchezo wao dhidi ya Ajax Amsterdam utakaopigwa baada leo ambapo watalazimika kushinda mchezo huo ili kufufua matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya timu 16 bora katika michuano hiyo. Pamoja na kuwa na wachezaji walionunuliwa kwa pesa nyingi mabingwa hao wa Ligi Kuu nchini Uingereza wamekuwa wakisuasua barani Ulaya baada ya kushindwa kupata ushindi katika michezo mitatu walioyocheza na kujikuta wakishika mkia katika Kundi D ambalo pia lina timu za Real Madrid na Borrusia Dortmund. Akihojiwa mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya West Ham United ambao City ilitoka sare ya bila ya kufungana, Mancini amesema kuwa hadhani kama kikosi hicho kipo tayari kushinda taji la ligi ya mabingwa kwasasa. Meneja huyo aliendelea huku akiwatolea mfano Chelsea kwamba wamesubiri kwa kipindi cha miaka 10 ndio wakaja kunyakuwa taji hilo msimu uliopita hivyo hata kwa City haitakuwa kazi rahisi haswa ikizingatiwa kundi gumu walilopangwa msimu huu na msimu uliopita. City ilianza michuano hiyo kwa kukubali kipigi cha mabao 3-2 kutoka kwa Madrid kabla ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Dortmund na baadae kupokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Ajax nchini Uholanzi. 

No comments:

Post a Comment