Monday, November 5, 2012
VILLA ALIKUWA HATARINI KUKATWA MGUU - DAKTARI.
DAKTARI ambaye aliyemtibu mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona, David Villa baada ya kuvunjika mguu wakati wa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia 2011 iliyofanyika nchini Japan amesema kuwa nyota huyo alikuwa katika hatari ya kukwata mguu wake. Daktari huyo aitwaye Ramon Cugar amesema kuwa nyota huyo mwenye umri miaka 30 angeweza kupoteza mguu wake kutokana na mabadiliko ya ghafla ambayo yangechangiwa wakati akisafiri na ndege muda mfupi baada ya kupata mejraha hayo. Cugar amesema kuwa mabadiliko makubwa ya msukumo aliyopata mchezaji huyo wakati akisafiri kwa ndege yangechangia kuongeza ukubwa wa tatizo na kupelekea mchezaji huyo kupoteza mguu wake. Daktari huyo alimsifu kocha wa Barcelona Tito Vilanova kwa kutoharakisha kumrejesha katika kikosi chake Villa ambaye pia amewahi kucheza katika klabu ya Valencia kwani kwa kufanya hivyo kumemfanya nyota huyo aweze kupona kwa asilimia 100.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment