Monday, November 5, 2012

MWAMUZI CLATTENBURG AACHWA TENA.

MWAMUZI wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Mark Clattenburg ameachwa tena katika orodha ya waamuzi ambao watachezesha mechi za ligi hiyo ambazo zitapigwa mwishoni mwa wiki hii. Clattenburg yupo katika uchunguzi wa polisi na Chama cha Soka cha nchi hiyo-FA kufuatia tuhuma za kutumia lugha ya kibaguzi kwa kiungo wa Chelsea John Mikel Obi wakati wa mchezo dhidi ya Manchester United wiki iliyopita. Mwamuzi huyo anatakiwa kuhojiwa na polisi pamoja na FA wiki hii baada ya malalamiko kuwasilishwa polisi na Chama cha Mawakili Weusi. Meneja Mkuu wa Chama cha Waamuzi wa Kulipwa nchini humo, Mike Riley amesema kuwa walikuwa wamepanga kumtumia Clattenburg mwishoni mwa wiki hii hata hivyo walipozungumza naye waliona ni busara kumpumzisha ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo.

No comments:

Post a Comment