Monday, November 5, 2012
VILABU BORA: BARCELONA YAONGOZA DUNIANI, ESPERANCE YAONGOZA AFRIKA.
SHIRIKISHO la Kimataifa la Soka la Historia na Takwimu-IFFHS ambalo linahusika na utunzaji wa historia na kumbukumbu za soka limetoa orodha ya mwezi Octoba mwaka huu ya vilabu 400 bora duniani. Katika orodha hizo klabu ya Barcelona bado imeendelea kukaa kileleni ikiwa na alama 349 ikifuatiwa na klabu ya Atletico Madrid wakishika nafasi ya pili wakiwa na alama 290 huku ya tatu ikiwa klabu ya CD Universidad de Chile Santiago ambayo imedondoka nafasi moja kutoka nafasi ya pili waliyokuwepo msimu Septemba mpaka nafasi ya tatu. Klabu nyingine ni Boca Juniors ya Argentina ambayo nayo imeshuka kwa nafasi moja kutoka ya tatu waliyokuwepo Septemba wakiwa na alama 276 na tano bora inafungwa na Real Madrid ambayo imejikusanyia alama 271. Kwa upande wa Afrika klabu ya Esperance ya Tunisia bado imeendelea kuongoza wakiwa nafasi ya 61 wakifuatiwa na Al Hilal Omdurman ya Sudan ambao wako nafasi ya 82 huku klabu nyingine ya Sudan Al-Merreikh Omdurman ikifuatia katika nafasi ya tatu kwa upande wa Afrika na 117 duniani. Chelsea Berekum ya Ghana inashika nafasi ya nne kwa upande wa Afrika huku duniani nayo pia ikishika nafasi ya 117 na tano bora inafungwa na Wydad Casablanca ya Morocco ambayo iko katika nafasi ya 141 duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment