Tuesday, November 6, 2012
FAINALI YAZUIA UWANJA WA BANGKOK FUTSAL ARENA KUTUMIWA KWA FAINALI YA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIANI LA NDANI NCHINI THAILAND.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA wameamua kutelekeza mpango wa kuandaa mchezo wa fainali ya michuano ya Soka ya Kombe la Dunia la Ndani wiki ijayo baada ya uwanja ambao umeigharimu Thailand dola milioni 40 kushindwa kukamilika kwa wakati. Katika taarifa yake FIFA imesema kuwa uwanja huo wa Bangkok Futsal Arena hautakuwa salama kwa timu pamoja na mashabiki ambao wanatarajiwa kuhudhuria fainali ya michuano hiyo. Sehemu ya kuchezea katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 12,000 iliwekwa baada ya michuano hiyo kuanza wiki iliyopita lakini utendajikazi wa huduma za msingi na vifaa mpaka sasa havijakamilika. FIFA wamesema kuwa mchezo wa fainali ambao utapigwa Novemba 18 mwaka huu na mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo itapigwa katika Uwanja wa Ndani wa Huamark jijini Bangkok huku ule war obo fainali ukichezwa katika Uwanja wa Ndani wa Nimibutr. Kamati ya maandalizi ya michuano hiyo nchini humo imelaumu mvua kubwa na mafuriko kuwa ndio chanzo kikubwa cha kuchelewa kukamilika kwa wakati kwa uwanja huo wa Bangkok Futsal Arena.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment