MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson ametajwa kuwa meneja bora wa mwezi Octoba na kupokea zawadi hiyo wakati wa sherehe za kutimiza miaka 26 akikinoa kikosi hicho chenye maskani yake Old Traford. Tuzo hiyo amepewa baada ya kuiwezesha timu yake kushinda mechi ngumu tatu mwezi ulipopita ambazo ni dhidi ya Newcastle United, Stoke City na Chelsea na kwasasa klabu hiyo ndio wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Kiungo nyota wa Chelsea Juan Mata ambaye amefunga mabao matatu mwezi uliopita ametunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Mbali na tuzo hiyo United wanapanga kutengeneza sanamu la kocha wao huyo ambalo litawekwa Old Traford Novemba 23 mwaka huu kuonyesha heshima kwa kocha huyo kwa mafanikio aliyoipa klabu hiyo katika kipindi chote ambacho amekuwepo hapo.
No comments:
Post a Comment