Wednesday, November 7, 2012
MAMA YAKE GYN APOTEZA MAISHA KATIKA AJALI.
NAHODHA wa timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan amepata msiba wa mama yake mzazi baada ya kupata ajali jijini Accra. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo mama yake Gyan aitwaye Cecilia Amoako ambaye ni mwalimu alishindwa kulimudu gari alilokuwa akiendesha na kugonga nguzo kabla ya kukimbizwa katika hospitali ya Ridge lakini alifariki muda mfupi kutokana na majeraha aliyopata. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kutoka kwa Gyan ambaye anacheza katika klabu ya Al Ain ya Falme za Kiarabu lakini mwili wa mama yake ulipelekwa katika chumba cha maiti cha hospitali hiyo. Kocha wa Ghana, Kwesi Appiah amekuwa wa kwanza kutuma salamu za rambirambi kwa mchezaji huyo na kumtakiwa moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu ambacho kinamkabili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment