Wednesday, November 7, 2012
MANCINI ACHUKIZWA NA MWAMUZI.
MENEJA wa Manchester City, Roberto Mancini ameonyesha kuchukizwa na mwamuzi baada ya kikosi chake kushindwa kutamba katika uwanja wa nyumbani na kutoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ajax Amsterdam katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa jana usiku. Mancini amemtuhumu mwamuzi Peter Rasmussen kwa kukataa bao lililofungwa kwa juhudi binafsi za Sergio Aguero katika dakika za lala salama kabla ya kulalamikia faulo aliyochezewa Mario Balotelli ambayo ingeweza kuwa penati kama mwamuzi angekuwa makini. Hatahivyo sare waliyopata City imeweka matumaini ya kusonga mbele lakini watahitaji kushinda michezo yao miwili iliyobakia dhidi ya Real Madrid watakaocheza nyumbani na Borussia Dortmund watakaocheza ugenini huku wakiomba matokeo mengine yaende kama wanavyotaka. Mancini amesema kuwa wakishinda michezo yao iliyobakia watakuwa na alama nane na kama wakifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora kwa alama hizo wanaweza kushinda taji la Ligi ya Mabingwa kitu ambacho kwa mahesabu ya haraka haraka kitakuwa kigumu kwao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment